KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Monday, April 11, 2016

Watumishi hewa wamponza mkuu wa Mkoa

Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wafanye uchunguzi kuwatambua watumishi hewa
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.

Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.

Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.

Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini ambapo jumla ya wafanyakazi 2,000 wamegunduliwa nchini Tanzania kwa awamu ya kwanza jambo ambalo Rais Magufuli anataka limalizwe mara moja.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.

"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt Magufuli.

Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.


Chanzo: bbc swahili

Friday, April 8, 2016

Uliwahi kuona Teja akiibiwa na kibaka?

Mwenye jaketi la njano ni kibaka na waliomkwida ni mateja wakimvuta kumpeleka polisi. Hapa ni mkabala na jengo la NSSF Manispaa ya Iringa


 KUNA usemi usemwao “mwizi akiibiwa, polisi hawalali”. Usemi huu si wakudhania wala wakufikirika.

Ilikuwa majira ya saa 6:27 mchana nilipowaona watu wakivutana mashati katikati ya barabara mkabala na jingo la Tanesco Manispaa ya Iringa hali ambayo kwa haraka sikuelewa.

Niliamua kusogea karibu kuuliza kinachoendelea nikaambiwa kibaka kamuibia teja ikabidi mateda wamkamate ili waanze kumshughulikia.

Mateja hao walimvuta kibaka huyo ng’ambo ya barabara wakampa kichapo kasha wakamkuda kuelekea naye kituo cha Polisi.

Wakati wakielekea kituo cha polisi kibaka akawa anaomba msamaha lakini mateja hao hawakutaka kumsikiliza zaidi ya kumchapa na kumsukuma kuelekea kituo cha polisi.

Haikuwa kazi rahisi kwa kibaka huyo kujieleza kwa kwa kuwa mateja hawakuta kusikia maelezo bali walitaka afikishwe mahakamani na kasha walihakakisha wanafka kituo cha polisi na kutiwa mikononi mwa polisi ili kazi ibaki kwa polisi

Wednesday, March 30, 2016

Waziri Mahiga akosolewa kutowaweka wazi watanzania juu ya fedha za MCC





Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje Mch. Peter Msigwa akiongea na waandishi wa habari juu ya fedha za MCC.



SIKU chache baada ya Serikali ya Marekani kuzuia fedha za msaada kwa ajili ya maendeleo Millennium Challenge Cooperation (MCC), msemaji kambi rasmi ya upinzani Waziri kivuli wa Wizara wa Mambo ya Nje Mch. Peter Msigwa ametoa tamko la kuwataka Jumuiya ya Ulaya nayo kuzuia misaada kwa serikali Tanzania iweze kujitafakari kama imezingatia vigezo vya MCC katika kupata misaada.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hotel ya M. R, Mch. Msigwa ambaye pia ni Mbubge wa Jimbo la Iringa Mjini alisema kambi ya upinzani imesikitishwa na maelezo ya Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Agustino Mahiga kutowaeleza wazi watanzania sababu hasa ya serikli ya Marekani kusitisha utolewaji wa fedha hizo za msaada badala yake kukurupuka na kutoa sababu ambazo hazina mashiko kwa wananchi.

Amesema kuwa sababu ambazo Balozi Mahiga alizitoa juzi hazina mashiko kwa kuwa serikali ya Tanzania imekiuka misingi mojawapo inayozingatiwa na MCC katika vigezo 17 katika kuchagua nchi inayostahili kupata msaada na miongoni mwa vigezo vya msingi kabisa ni nchi husika kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha demokrasia na kuendesha chaguzi zilizo huru na haki.

Amesema kuwa katika taarifa yake MCC ilieleza maeneo ambayo Tanzania imekiuka vigezo kuwa ni marudio ya uchaguzi haramu wa urais Zanzibar na kupitisha Sheria ya Makosa ya Mawasiliano ya Mitandaoni (Cyber Crime) sheria inayonyima uhuru wa wa kujieleza na uhuru wa kujumuika.

"Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa sheria ya Uhalifu wa Mtandao , Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa”, amesema

Mchungaji Msigwa amesema kuwa kwa mantiki hiyo ni dhahiri kuwa Tanzania haikupaswa kushitushwa na uamuzi wa MCC kwa kuwa Serikali ilivifahamu vizuri na mapema vigezo vya kustahili kupewa misaada na MCC.

Aliongeza kuwa inashangaza na kusikitisha kuona Msomi na Mwanadiplomasia mzoefu kama Balozi Mahiga akilitia Taifa Aibu ya Mwaka kwa kulalamikia kuonewa na kutoa kauli za “hovyo” kama alivyozitoa.

Saturday, March 26, 2016

Binadamu amejipaka uchafu: Askofu Ngalalekumtwa




BINADAMU anaelezwa kuwa ni kiumbe kilichochafuka na uchafu wa kutisha ambao anahitaji msaada kwa ajili ya kusafishwa.

Haya yamezungumzwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa akihubiri katika Mkesha wa Pasaka Parokia ya Bikira Maria Consolata - Mshindo Jimbo la Iringa.

Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa alisema binadamu amejaa maovu ya kila aina ambayo yamekuwa kikwazo kwa wengine na kusema kuwa bila nguvu ya Mungu mwanadamu pekee hayawezi.

Thursday, March 10, 2016

Baada ya mgogoro wa uchaguzi Uganda, waandishi wa habari wanahofia usalama wao wa kihabari




Yoweri Kaguta Museven
Mpiga picha wa muda mrefu nchini Uganda Abubaker Lubowa ametoa hisia zake jinshi ilivyomgharimu baada ya kupewa kazi na mhariri wake kuripoti habari za mpinzani wakati wa kampeni katika uchaguzi Mkuu Uganda akimripoti kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Mwezi Februari 27,  Mwaka hu, Lubowa na mwenzake katika gazeti binafsi la Daily Monitor walikamatwa wakiwa katika harakati za kuandika habari za  kiongozi wa upinzani Besigye mji mkuu wa Uganda, ambapo Besigye amefungiwa tangu matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa Februari 20.

Saturday, February 27, 2016

Rushwa yabadilishwa jina sasa yaitwa "mipango"


WAKATI Serikali ya awamu ya tano ikija na neon utumbuaji majipu, baadhi ya watendaji wamekwepa kuita rushwa au takrima na kubuni jina linguine kuwa ni “mipango”.

Mtandao huu umeshuhudia baadhi ya maofisa watendaji wakitaka kupa fedha kutoka kwa mwanamke mmoja aliyekuwa akijenga kiti cha nyumba katika mtaa wa Igumbilo Kata ya Ruaha katika Manispaa ya Iringa wakidai kuwa za mipango.

Wakati watendaji hao wakimkomalia mwanamke huyo ili awapatie fedha, walikuwa wakitumia kigezo kuwatamsimamisha asiendelee na ujenzi kwa sababu ya kutokuwa na kibali.

Wakati wakiendelea kumkomalia mama huyo mtandao huu ulitaka kujua kama hizo fedha ambazo angezitoa mama huyo zinatolewa stakabadhi na kama ni za kisheria lakini ofisa mtendaji wa mtaa huo Ashery Msigala alisisitiza kuwa ni kwa ajili ya mipango.

“Siku zote ukitaka kufanikiwa kwa haraka lazima uwe na mipango. Ukitaka kufanyiwa kazi yako kwa haraka zaidi lazima uwe na mipango.

“Unapoamka kwenda ofisi ya mtu kwa ajili ya kupata huduma, ili huduma hiyo iweze kwenda kwa haraka zaidi lazima unapoondoka uwe na mipango kama hamasa kwa mtendaji unayekwenda kuonana naye ili akusaidie” amesema Msigala.

BAADHI YA WAAJIRI WANAWANYANYASA WAFANYAKAZI WANAPOJIUNGA NA VYAMA VYAO



BAADHI ya waajiri wanalalamikiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wao pindi wanapojiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuwakatisha moyo wa kutafuta haki zao.

Haya yamezungumzwa na Mohamed Sadick alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Kanda wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi zingine (TAMICO) uliofanyika katika ukumbi wa jengo la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Iringa.

Sadick amesema kazi ya vyama vya wafanyakazi si ndogo kwa kuwa hufanya kazi zaidi ya vyama vya siasa kwa kudai haki ya kweli kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali bila kujali idikadi na bila ubaguzi wowote.

Amesema pamoja na kuwa wafanyakazi wana haki mbalimbali kazini, wapo baadhi ya waajiri ambao huwatishia wafanyakazi wao pale wanapojiunga na vyama vya wafanyakazi wakitaka kuwakatisha tamaa ya kudai haki zao ili waendelee kunyonywa.