Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.
Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
Awamu
ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu
na Shinyanga Vijijini ambapo jumla ya wafanyakazi 2,000 wamegunduliwa
nchini Tanzania kwa awamu ya kwanza jambo ambalo Rais Magufuli anataka
limalizwe mara moja.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema
amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala
wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.
"Na wale
wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa,
walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana,
na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko
makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema
Dkt Magufuli.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment