WATU 50 wamepoteza maisha katika
ajali ya basi kampuni ya Majinja lililokuwa likitikea jijini Mbeya kwenda
jijini Dar es Salaamu katika maeneo ya Changarawe nje kidogo na mji mdogo wa Mafinga.
Ajali hiyo iliyo iliyo husisha basi
lenye namba za usajili T 438 CDE na lori lililokuwa limebeba kontena lenye namba
za usajili T 966AFA, basi lilianguka liliingia kwenye shimo na kupoteza
mwelekeo kisha kuanguka hali iliyosababisha lori lililokuwa likipishana na basi
hilo kuingia kwenye shimo hilo kisha kuanguka na kontena kulakia basi.
Mtandao huu umeshuhudia eneo la tukio
kontena hilo likiondolewa kwenye basi huku maiti zikinasuliwa na kwamba magari
yote yalikuwa katika mwendo kasi huku kila mmoja akitakakumuwahi mwenzake
katika shimo hilo.
“Kila dereza alitaka kumuwahi mwenzake
katika shimo hilo lakini kwa bahati mbaya basi likaingia kwenye shimo hilo
likahama kisha kuanguka na roli nalo likafuata nalo likaanguka na kontena
likalalia basi” alisema shuhuda.
Katika ajali hiyo ni mtoto anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka mitatu alitoka akiwa mzima huku dereva wa lori akikimbia
baada ya ajali.
Akiongea na waandishi wa habari nje ya
hospitali ya Wilaya Mafinga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema watu
42 wamefariki na wengingine 22 wamejeruhiwa.
Mtandao huu ukishuhudia katika eneo la
tukio, watu wanne wameokolewa wakiwa hai
na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya Mafinga ambapo nao wamefariki baada ya
kufikishwa hospitalini.
Wananchi wameelekeza lawama zao kwa
TANROAD kuwa wameshindwa kufukia shimo hilo licha ya kuwepo kwa muda mrefu.
Meneja wa Tanroad Mkoa wa Iringa Paul
Lyakulwa alipotafutwa na mtandao huu ili kutolea maelezo juu ya shimo hilo
alisema wanaandaa taarifa ya pamoja.
“Tutakaa na Mkuu wa Mkoa ili tuandae
taarifa ya pamoja” alisema Lyakulwa.
Hata hivyo mbele ya shimo hilo, shimo la
mbele yake lilisababisha ajali ya gari dogo hapo jana.
Wananchi wa Mafinga wanasema ajali hiyo
ni kubwa na ya kwanza kutisha katika eneo hilo.
Ni mara ya pili kwa kampuni ya Majinja
kupata ajali katika eneo la Changarawe ambapo mwishoni mwa mwaka jana basi la
kampuni hiyo lilipata ajali karibu na hospitali ya Wilaya Mafinga japo kuwa
hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment