KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Saturday, July 25, 2015

Matokeo ya kura za maoni Chadema kwa baadhi ya majimbo






JIMBO la Kilolo kwa mara ya kwanza limefanya upigaji wa kura za maoni kupitisha mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo wajumbe wamejivunia kumpata mgombea shupavu anayejiamini na kwamba ana nguvu kubwa ya kushinda katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu.

Katika uchaguzi huo jumla ya wapiga kura walikuwa 240 ambapo Brian Kikoti aliibuka kwa ushindi wa kura 215, Ahaz Challi 12, Samson Mnyawami  9, Edger Kihwelo 2, Hezlon Lusapi 2.

Mufindi Kusini: Frank Malata 69, Oliva Lema 27, Crepton Madunda 18 Mustafa Msovera 12 jumla ya kura 126.

Jimbo la Isimani: Patrick Ole Sosopi 101, Widmani Masika 31 jumla ya kura zote ni 142 wakati Iringa Mjini: Mch. Peter Msigwa 177, Leonce Marto 18 huku kura 1 ikiharibika na jumla ya kura zote 196.

Kwa upande wa Jimbo jipya la Mafinga; Jeofrey Mungai ameibuka mshindi.

Ludewa: Okol Haule 181, Batromeyo Mkinga 126, David Msanga 3. Njombe Kusini: Emmanuel Masonga 92, Emilian Msigwa 41, Fukh Lulandala 13, Ally Mhagama 3, Alatanga Nyagawa 1, Stanislaus Mdetele 2,  Emmanuel Filangali 1, Lucia Mlowe 0. Viti maalum Rose Mayemba.

Makete: Jackson Mbogela 143, Ahadi Mtweve 77, Meck Emmanuel  9, Hadson Mrema 8, Benjamini Bukuku 1, Abiud Mwandikilwa 0.

Akihutubia mara baada ya kutangazwa mshindi kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Kilolo Brian Kikoti alisema kwa ushindi alioupata ameamini kuwa anahitajika na kwamba anayo kazi ya kufanya ili asiwaangushe wajumbe waliompigia kura na wananchi kwa ujumla.

“Mmenionesha kuwa mnanihitaji. Tunakwenda kushinda uchaguzi katika ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais. Sitawaangusha ndugu zangu” alisema Kikoti.

No comments:

Post a Comment