KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Thursday, March 10, 2016

Baada ya mgogoro wa uchaguzi Uganda, waandishi wa habari wanahofia usalama wao wa kihabari




Yoweri Kaguta Museven
Mpiga picha wa muda mrefu nchini Uganda Abubaker Lubowa ametoa hisia zake jinshi ilivyomgharimu baada ya kupewa kazi na mhariri wake kuripoti habari za mpinzani wakati wa kampeni katika uchaguzi Mkuu Uganda akimripoti kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Mwezi Februari 27,  Mwaka hu, Lubowa na mwenzake katika gazeti binafsi la Daily Monitor walikamatwa wakiwa katika harakati za kuandika habari za  kiongozi wa upinzani Besigye mji mkuu wa Uganda, ambapo Besigye amefungiwa tangu matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa Februari 20.


Februari 22 katika eneo moja, Lubowa na mwingine mpiga picha, Isaac Kasamani wa Kifaransa wa shirika la habari la Agence France-Presse (AFP), walishambuliwa na watu waliokuwa wamevaa sare za polisi na kupigwa mabomu ya machozi.

Hata hivyo Kasamani alifanikiwa kujikinga katika na mabomu hayo lakini Lubowa aliweza kutoroka-kama alivyofanya Novemba 16 wakati mwenzake mwingine, Isaac Kugonza, akipata mateso makali na kichwa kupasuka katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi.


Kwa muda mrefu waandishi wa Uganda wamekuwa wakishambukliwa na kunyanyaswa pamoja na vyombo vya habari vikinyanyaswa.

No comments:

Post a Comment