Mwenye jaketi la njano ni kibaka na waliomkwida ni mateja wakimvuta kumpeleka polisi. Hapa ni mkabala na jengo la NSSF Manispaa ya Iringa |
KUNA usemi usemwao “mwizi akiibiwa,
polisi hawalali”. Usemi huu si wakudhania wala wakufikirika.
Ilikuwa majira ya saa 6:27 mchana
nilipowaona watu wakivutana mashati katikati ya barabara mkabala na jingo la
Tanesco Manispaa ya Iringa hali ambayo kwa haraka sikuelewa.
Niliamua kusogea karibu kuuliza
kinachoendelea nikaambiwa kibaka kamuibia teja ikabidi mateda wamkamate ili
waanze kumshughulikia.
Mateja hao walimvuta kibaka huyo ng’ambo
ya barabara wakampa kichapo kasha wakamkuda kuelekea naye kituo cha Polisi.
Wakati wakielekea kituo cha polisi
kibaka akawa anaomba msamaha lakini mateja hao hawakutaka kumsikiliza zaidi ya
kumchapa na kumsukuma kuelekea kituo cha polisi.
Haikuwa kazi rahisi kwa kibaka huyo
kujieleza kwa kwa kuwa mateja hawakuta kusikia maelezo bali walitaka afikishwe
mahakamani na kasha walihakakisha wanafka kituo cha polisi na kutiwa mikononi
mwa polisi ili kazi ibaki kwa polisi
No comments:
Post a Comment