Baadhi watoto wa kituo cha Huduma ya Mtoto na waalimu wao wakipokea msaada kutoka club ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Iringa |
CLUB ya inayoshughulika na
masuala ya Virus vya Ukimwi na UKIMWI yaa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo
cha Mkoa wa Iringa kimetoa msaada katika kituo cha kulea watoto yatima cha
Huduma ya Mtoto kilichopo Ilula Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa.
Akikabidhi msaada huo kituoni hap, mlezi
wa kikundi hicho ambaye pia ni mhadhiri wa chuo hicho Festogrands Chikungua
alisema suala la kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni la
jamii nzima na kwamba jamii itambue jukumu hilo na kuwasaidia watoto kama hao
ambao hawana msaada mwingine kwa ajili ya kujenga maisha yao ya baadaye.
Pia amesema watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi hawakupenda kuishi katika mazingira hayo jambo
linaloweza kumpata mtu yeyote kuiacha familia yake.
“Hawa watoto ni wetu.
Tunapaswa kuwahudumia na kuwalea kama tufanyavyo watoto wetu. Tuwajibike kwa
pamoja kuwalea na kuwapa mahitaji stahiki bila kinyongo, ubaguzi au chuki.
“Watoto hawa hawakupenda kuwa
katika mazingira waliyopo. Hivyo, tukumbuke kuwa na sisi tupo safarini na
tunafamilia. Tushirikiane kuwalea hawa watoto ili hata wao waweze kuwa msaada
kwa wengine hapo baadaye” amesema.
Chikungua amewaasa watoto hao
wakazane na kuzingatia masomo na malezi wapatayo ili waweze kufikia malengo yao
kwa ajili ya maisha yao ya badaaye.
“Tumieni nafasi hii katika
kuandaa maisha yenu. Zingatieni masomo kwa bidii, malezi na uadilifu ili muweze
kuyafikia malengo yenu” amesema.
Akipokea msaada huo,
Mkurugenzi wa kituo hicho Baraka Kibungu amesema hatua iliyofikiwa na Chuo
Kikuu Huria kituo cha Iringa iwe mfano wa kuigwa na jamii na kuitaka jamii
kufuata mfano huo.
Kibungu amesema kuwa kituo
hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwe ya kuwa na uhaba wa madarasa
na vyoo, na kwamba watu wenye mapenzi mema wajitokeze kutoa msaada wa hali na
mali ili kuwezesha kutatua matatizo hayo.
Kituo hicho nyenye usajili
namba T 903 kinachomilikiwa na Kanisa la Pentekoste Tanzania kwa ushira wenza
na Compassion International Tanzania chenye jumla ya watoto 252 wakiwemo
wavulana 120 na wasichana 132 kilianzishwa mwaka 2010 ambapo kina jumla ya wali
14.
Kikundi cha Chuo Kikuu Huria
kilitoa msaada wa vyakula ikiwemo kilo 50 za sukari, mafuta ya kula lita 10,
chumvi katoni 2 na unga wa sembe kilo 250.
No comments:
Post a Comment