WANANCHI wa Mufindi katika Mkoa Iringa wapo
katika taharuki kubwa na hofu ya kuvamiwa na simba kutokana na wanayama hao
kupita katika maeneo mengi katika makazi yao.
Haya yamezungumzwa leo na mwenyekiti wa
Kijiji cha Ndolezi Kata ya Boma katika wilaya ya Mundi, Clement Nditu
alipokukuwa akiongea na mtandao huu juu ya taharuki inayokikumba kijiji
chake.
Nditu amesema wanakijiji waligundua kuwa
wapo hatarini walipokuwa wakienda mashambani mwao na kuona nyayo za mnayama
wasiyemfahamu jambo lililowalazimu kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ili
hatua za kiusalama zifuate.
Maelezo ya mwenyekiti wa kijiji hicho
yanakuja baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kijiji cha Ndolezi kimevamiwa na
simba japo kuwa haikuelezwa kama kuna madhara yoyote kwa wananchi.
Mtandao huu umemtafuta ofisa mtendaji
wa kijiji hicho Yohana Kikungwe ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi ambapo amesema
kijiji hicho na maeneo jirani katika Kata hiyo wapo katika sintofahamu ya
hatima ya wanayama hao.
Taharuki hiyo ilianza Jumamosi 14,
Machi mwaka huu katika kijiji cha Luganga kinachopakana na Kata ya Ifwagi baada
ya wananchi kubaini kuwa huenda wameingiliwa na wanyama wakali katika maeneo
yao baada ya kuona nyayo.
“Tangu Jumamosi iliyopita katika maeneo
ya Luganga tulipata taarifa kwa wananchi kuwa wanaona nyayo ambazo si za
kawaida na kututaka kufanya uchunguzi. Lakini kwa kuwa mimi si mtaalamu wa
wanyama, niliwasiliana na wataalamu wa wanyama pori ili waweze kufika
kutusaidia.
“Wataalamu wa wanayama pori walikuja na
kutujulisha kuwa ni nyayo za simba ambapo walipiga kambi siku tatu wakiwafuatilia
lakini hawakuwaona ikabidi waondoke na kuwaomba wananchi watakapowaona sehemu
yoyote watoe taarifa” amesema Kikungwe.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa siku
ya juzi wanyama hao walionekana katika kijiji cha Kibao.
Katika hatua nyingine taarifa zilizotufikia
jana asubuhi zilieleza kuwa wanyama hao walionekana katika maeneo ya soko la
Mafinga na kusambazwa kwa taarifa sehemu
mbalimbali kwa wananchi ili waweze kuwa na tahadhari.
Ubisimbali alisema bado wanaendelea na
msako wa wanyama hao na kwamba wananchi wanapaswa kutoa taarifa za haraka pindi
wanapowaona wanyama hao sehemu yoyote ili waweze kudhibitiwa kabla hawaleta
madhara.
“Nimelisikia na ninalifahamu suala la
simba kuvamia maeneo ya makazi ya watu. Katika maeneo ya Luganga na leo asubuhi
tumesikia ni Mafinga sokoni, tukafika hapo sokoni tukahojiana na wananchi na
tukawaambia kama watawaona popote watutaarifu japo kuwa wataalamu wetu
wameingia porini kuwatafuta.
“Tunawaomba wananchi wakae katika hali
ya tahadhari kwa sababu hawa simba hawajapatikana kwa hiyo wanaweza kufika au
kuonekana tena sehemu nyingine kwa sababu wanatembea na kuhama hama. Tusaidiane
kwa hili ili wasilete madhara. Wasijisahau kwa kuwa wataalamu wetu wapo huko
kuwatafuta kwani hawa wananyama wanatembea” amesema.
Tangu kupatikana kwa taarifa za kuwapo
kwa wanyama hao wakali, haijaripotiwa taarifa yoyote ya madhara yanayotokana na
wanayama hao na hali ya taharuki kwa wananchi bado inaendelea kwa kuwa wanayama
hao wanaendelea kuonekan sehemu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment