Maandamano ya upinzani yanafanyika
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya
kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani
baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa
mwaka huu.
Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo
mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa
Upinzani Moise Katumbi.
Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi
kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba
jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi
huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya
Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa
kwenda kazini.
Mjini Goma katika eneo la Birere,amesema kuwa ni mchezo wa paka na
panya ambapo vijana wamekuwa wakijibizana na polisi kwa kuwarushia mawe
huku nao maafisa hao wakiwatupia vitoa machozi.
Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi.
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment