Vyombo vya habari nchini Marekani,
vinaripoti kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary
Clinton ameshinda uteuzi wa chama hicho katika eneo la Puerto Rico.
Ushindi
huo unaimarisha matumaini yake ya kunyakua uteuzi wa chama hicho,
katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Matokeo
ya awali yanaashiria kuwa Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura
ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Bi Clinton sasa anahitaji chini ya wajumbe 30tu ili kushinda uteuzi wa chama hicho.
Ushindi
huo ni afueni kubwa kwa Bi Clinton huku wakipiga kura katika majimbo ya
New Jersey na California wakiajianda kupiga kura siku ya Jumanne.
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment