Umri wa kuishi barani Afrika
unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani
kulingana na shirika la afya dunia WHO.
Ripoti ya WHO inasema
tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10
zaidi.Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.
Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.
Daktari
Ties Boerma kutoka WHO ameimbia Newsday kwamba sababu moja ni kupungua
kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.
Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:
Algeria - 75.6
Tunisia - 75.3
Mauritius - 74.6
Morocco - 74.3
Cape Verde - 73.3
Seychelles - 73.2
Libya - 72.7
Egypt - 70.9
Sao Tome - 67.5
Senegal - 66.7
Taifa
la Ethiopia ni la 16 katika orodha hiyo likiwa na kiwango cha kuishi
cha wastani wa miaka 64.8,Kenya ikiwa ya 22 na miaka 63.4,Ghana iko
katika nafasi ya 25 ikiwa na miaka 62.4,Somalia ni ya 47 ikiwa na miaka
55 na Nigeria ni ya 48 ikiwa na miaka 54.5.
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment