Huduma ya mabasi ya uchukuzi
yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne
katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Abiria watalipa
shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya
uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.
Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard
Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400
kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa
uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200
kwa kila safari.
ASiku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.
Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa
magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea
kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga
barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.
Kulingana
na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja
na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT
hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment