KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Tuesday, July 5, 2016

Setilaiti ya Juno yafika Jupiter

Satelite ya Juno kama inavyoonekana
Ile Setilaiti ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupiter imefika kwenye sayari hiyo na kuanza kuizunguka.

Wanasayansi wanakadiria setilaiti hiyo ilifika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za Afrika Mashariki.

Setilaiti hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.

Mawasiliano kutoka kwa chombo hicho cha juu yalipokelewa katika maabara ya Nasa eneo la Pasadena, California kwa shangwe.

"Vituo vyote vya Juno, tunapokea sauti ya kufanikiwa kwa chombo Delta B," kituo cha udhibiti wa Juno kilitangaza. "Roger Juno, karibu Jupiter."
Chombo cha Juno kikipaa
Wanasayansi wanatarajiwa kutumia chombo hicho kufahamu Zaidi muundo wa sayari ya Jupiter ambayo hujulikana kwa Kiswahili kama Zohali.

Wanafikiri muundo wake kikemia unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi sayari hiyo iliundwa miaka bilioni nne unusu iliyopita.

Hakuna chombo cha anga za juu kilichowahi kufika karibu sana na sayari hiyo kama kilivyofanya chombo cha Juno.

Miali nururishi kutoka kwa sayari hiyo huwa na uwezo wa kuharibu vyombo vya kielektroniki visivyokingwa vyema.

Chombo vya Juno kimezingirwa na kinga ya madini ya Titanium.

Kwa sasa Juno itakuwa ikichukua siku 53 kuizunguka sayari hiyo.

Baadaye Oktoba, itaongeza kasi na kuikaribia zaidi sayari hiyo na kuanza kutumia siku 14 kumaliza mzunguko.
Lengo kuu litakuwa kubaini iwapo kuna oksijeni katika sayari hiyo. Hii sana itakuwa imefungamanishwa na maji, iwapo yapo.

"Kiwango cha maji katika sayari ya Jupiter kitatueleza mengi kuhusu ni wapo sayari hiyo ilikuwa ilipoundwa mapema katika mfumo wa jua,” anasema mmoja wa wanasayansi wanaohusika katika mradi huo Candy Hansen.

"Tunafikiri kwamba Jupiter iliundwa ikiwa pahala tofauti na ilipo sasa."
  • Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.



Chanzo: bbc swahili

Tuesday, June 21, 2016

Ghasia mbaya zashuhudiwa Afrika Kusini

Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.

Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.

Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.

Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.

Serikali ya Afrika Kusini imeomba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.


Chanzo: bbc swahili

Thursday, June 9, 2016

Watoto 6 wafa wakibatizwa Zimbabwe

Robert Mugabe
Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe.

Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake ni ya baridi; watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.

Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu hilo la Kikristo.

Lakini pia walimjumuisha mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake .



Chanzo: bbc swahili

Monday, June 6, 2016

Hillary ashinda jimbo la Puerto Rico

Hillary ashinda eneo la Puerto Rico
Vyombo vya habari nchini Marekani, vinaripoti kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda uteuzi wa chama hicho katika eneo la Puerto Rico.

Ushindi huo unaimarisha matumaini yake ya kunyakua uteuzi wa chama hicho, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.

Matokeo ya awali yanaashiria kuwa Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Bi Clinton sasa anahitaji chini ya wajumbe 30tu ili kushinda uteuzi wa chama hicho.

Ushindi huo ni afueni kubwa kwa Bi Clinton huku wakipiga kura katika majimbo ya New Jersey na California wakiajianda kupiga kura siku ya Jumanne.


Chanzo: bbc swahili

Thursday, May 26, 2016

Maandamano ya kumpinga Kabila yafanyika DRC

Waandamana Kumpiga kabila
Maandamano ya upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa Upinzani Moise Katumbi.

Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.

Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.

Friday, May 20, 2016

Chanjo imepunguza viwango vya watoto wanaofariki
Umri wa kuishi barani Afrika unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani kulingana na shirika la afya dunia WHO.

Ripoti ya WHO inasema tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10 zaidi.Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.

Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.

Daktari Ties Boerma kutoka WHO ameimbia Newsday kwamba sababu moja ni kupungua kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.

Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:

Walioua watu msikitini Mwanza wasakwa

Shambulio lilitekelezwa wakati wa swala jioni
Polisi nchini Tanzania wanawazuilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika shambulio katika msikiti mmoja mjini Mwanza magharibi mwa nchi hiyo.

Watu watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi jijini humo, Ahmed Msangi, uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia mapanga na kuongeza kuwa, polisi wanachunguza chanzo cha shambulizi hilo.

Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, wamesema shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wasiopungua 15.
Hakuna aliyedai kuhusika katika shambulio hilo.

Tukio jingine la mauaji ya kutumia silaha pia limetokea katika mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga ambapo askari polisi aliyefahamika kwa jina la Sajenti Kinyogoli ameuawa na watu wasiojulikana.

Matukio hayo yote yametokea wiki hii kulipoibuka taarifa kwenye mtandao wa Twitter juu ya kikundi kilichojitambulisha kama wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa Islamic State wakifanya mazoezi eneo la Tanga, kaskazini mashariki mwa Tanzania.


Chanzo: bbc swahili