Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa
ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa
polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao
kwa mawe.
Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na
suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC
kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeomba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment