Watoto sita wamekufa maji bila
kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini
Zimbabwe.
Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake
ni ya baridi; watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi
wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.
Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu hilo la Kikristo.
Lakini
pia walimjumuisha mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii ambaye
alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake .
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment