KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Saturday, March 14, 2015

TAKUKURU wataka wananchi wasikubali kuhongwa


TAASISI ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa iringa wamewataka wananchi kutokubali kuhongwa na wagombea wa uombozo katika kipindi hiki tunapoelekea katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Haya yamezungumzwa na ofisa wa TAKUKURU elimu kwa umma Iringa Anneth Mwakatobe alipokuwa akiongea na mtandao huu ofisini kwake.

Mwakatobe amewataka wananchi kutambua viashiria vya rushwa wakati huu kuwa ni pamoja na mgombea au mwanasiasa kutoa kitu kama khanga na vitenge kwa ajili ya kutaka kuchaguliwa ama kushawishi wananchi kumchagua mtu fualani.

“Mgombea akiwa nakusanya baadhi ya watu halafu anakutana nao kwa siri watu wengine kujua aidha kwa kutaka kuongea nao labda kutoa ahadi kwa watu, ahadi ambazo zinawashawishi watu kumchagua au kuwapa watu fedha ili wamchague ni rushwa.

“Pia mgombea ambaye hajiamini yaani mgombea ambaye hana maslahi ya taifa, mgombea ambaye hana sera lakini haoneshi kama ana nia ya dhati yaani anashawishi zaidi, huyo naye tunaweza kusema ana viashiria vya rushwa” amesema Mwakatobe.

Wednesday, March 11, 2015

Simanzi, ajali yaua watu 50




WATU 50 wamepoteza maisha katika ajali ya basi kampuni ya Majinja lililokuwa likitikea jijini Mbeya kwenda jijini Dar es Salaamu katika maeneo ya Changarawe nje kidogo na mji mdogo wa Mafinga.

Ajali hiyo iliyo iliyo husisha basi lenye namba za usajili T 438 CDE na lori lililokuwa limebeba kontena lenye namba za usajili T 966AFA, basi lilianguka liliingia kwenye shimo na kupoteza mwelekeo kisha kuanguka hali iliyosababisha lori lililokuwa likipishana na basi hilo kuingia kwenye shimo hilo kisha kuanguka na kontena kulakia basi.

Mtandao huu umeshuhudia eneo la tukio kontena hilo likiondolewa kwenye basi huku maiti zikinasuliwa na kwamba magari yote yalikuwa katika mwendo kasi huku kila mmoja akitakakumuwahi mwenzake katika shimo hilo.

“Kila dereza alitaka kumuwahi mwenzake katika shimo hilo lakini kwa bahati mbaya basi likaingia kwenye shimo hilo likahama kisha kuanguka na roli nalo likafuata nalo likaanguka na kontena likalalia basi” alisema shuhuda.

Katika ajali hiyo ni mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu alitoka akiwa mzima huku dereva wa lori akikimbia baada ya ajali.

Tuesday, March 3, 2015

Open University Iringa watoa msaada kwa waishio na VVU

Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Iringa (aliyeshika chupa) na walezi wa Clab ya chuo hicho (Open University HIV/AIDS Club) wakimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Alamano Sr. Rosela msaada wa vyakula kwa ajili ya kuwasaidia wanaoishi na VVU.



JAMII inapaswa kutambua na kujitoa katika kuwahudumia wanaoishi na VVU na kuwajali kwa kila namna ili waweze kuishi muda mrefu wakihudumia familia zao.

Haya yamezungumzwa leo na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria kituo cha Iringa Mch. Dkt. Lechion Peter Kimilike alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya kuwasaidia wanaoishi na VVU katika kituo cha Allamano kilichopo katika Manispaa ya Iringa.

Amesema kazi ya kuwahudumia waishio na VVU ni ya jamii nzima kwani hali hii inaweza kumtokea mtu yoyote na kwamba jamii isiwabague, kuwatenga au kuwafanyia vitendo vya kikatili wanaoishi na maambukizi bali iwafariji na kuwajali kwa kila jambo ili wasikate tama ya kuishi.

“Kazi hii ni yetu sote. Jamii inapaswa kutambua kuwa kuwafanyia vitendo vya ukatili watu kama hao ni dhambi na ni kosa kisheria.

“Ni dhamna potofu kuwafanyia vitendo vya ukatili watu kama hawa. Jamii iwe na uelewa wa kutosha” amesema Kimilike.

Dkt. Kimilike pia ameitaka jamii kutambua kuwa kuzaa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi si dhambi bali ni kiumbe kama walivyo wengine ambaye anapaswa kuishi na kupata mahitaji kama wapatayo wengine.

“Kuua albino ni wazo potofu na ni baya sana. Imani hii haikubaliwi wala haiwezi kuungwa mkono na mtu yeyote. Kuwaua watu kama hawa ni kutenda dhambi tu kwani hawa ni watu kama tulivyo wengine ambao wanapaswa kupewa haki zote” amesema.

Pia ameiasa jamii kutoa ushirikiano wa dhati katika kukemia vitendo vya ukatili na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kuwajibishwa kisheria.

Monday, March 2, 2015

Club ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Iringa yatoa msaada kituo cha watoto

Baadhi watoto wa kituo cha Huduma ya Mtoto na waalimu wao wakipokea msaada kutoka club ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Iringa
CLUB ya inayoshughulika na masuala ya Virus vya Ukimwi na UKIMWI yaa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Mkoa wa Iringa kimetoa msaada katika kituo cha kulea watoto yatima cha Huduma ya Mtoto kilichopo Ilula Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa.

Akikabidhi msaada huo kituoni hap, mlezi wa kikundi hicho ambaye pia ni mhadhiri wa chuo hicho Festogrands Chikungua alisema suala la kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni la jamii nzima na kwamba jamii itambue jukumu hilo na kuwasaidia watoto kama hao ambao hawana msaada mwingine kwa ajili ya kujenga maisha yao ya baadaye.

Pia amesema watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hawakupenda kuishi katika mazingira hayo jambo linaloweza kumpata mtu yeyote kuiacha familia yake.

“Hawa watoto ni wetu. Tunapaswa kuwahudumia na kuwalea kama tufanyavyo watoto wetu. Tuwajibike kwa pamoja kuwalea na kuwapa mahitaji stahiki bila kinyongo, ubaguzi au chuki.

“Watoto hawa hawakupenda kuwa katika mazingira waliyopo. Hivyo, tukumbuke kuwa na sisi tupo safarini na tunafamilia. Tushirikiane kuwalea hawa watoto ili hata wao waweze kuwa msaada kwa wengine hapo baadaye” amesema.

Chikungua amewaasa watoto hao wakazane na kuzingatia masomo na malezi wapatayo ili waweze kufikia malengo yao kwa ajili ya maisha yao ya badaaye.

“Tumieni nafasi hii katika kuandaa maisha yenu. Zingatieni masomo kwa bidii, malezi na uadilifu ili muweze kuyafikia malengo yenu” amesema.

Monday, February 23, 2015

WANASIASA NA WAFANYABIASHARA WAHUSISHWA NA MAUAJI YA ALBINO NCHINI TANZANIA


TATIZO la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino linalozidi kushika kasi nchini Tanzania linaelezwa kuwa linatokana na watu wenye uchu wa madaraka na mali ambao wamekosa maadili na hofu ya Mungu huku wanasiasa wakihusishwa na jambo hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu, wananchi wanaoneshwa kusikitishwa na vitendo hivyo huku wakiitupia lawama serikali kuwa inaonesha uzembe wa makusudi kulichukulia uzito suala hilo.

Sisto Khani mkazi wa Iringa mjini ameuambia mtandao huu kuwa, serikali imeonesha udhaifu katika suala hili kutokana na kutowachukulia hatua kali watuhumiwa wanaokamatwa kwa vitendo hivyo na kwamba kama serikali itaendelea kuonesha udhaifu wa namna hiyo, vitendo hivyo haviwezi kuisha.
Hata hivyo Sisto alisema pamoja na serikali kuonesha udhaifu katika suala hilo, ushirikina ndio chanzo kikubwa cha vitendo hivyo kutokana na watu kuamini kuwa kwa kutumia viungo vya watu hao unaweza kupata utajiri au kutimiza matakwa yao.

“Ushirikina na chanzo cha mauaji ya albino kwa sababu kuna watu wanatumia njia hiyo eti wanataka vyeo, utajiri, mali na uongozi” amesema.

Monday, February 16, 2015

Kesi ya mauaji ya Mwangosi yazidi kuunguruma katika Mahakama Kuu Iringa

KESI ya mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi inayomkabili Pasificus Cleophace Simon imeendelea kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu kanda ya Iringa ambapo mashahidi wawili upande wa Jamhuri waliweza kutoa ushahidi wakiongozwa na wawendesha mashtaka wa serikali Sunday na Ladslaus Komanya.

Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Paul Kihwelo shahidi namba tatu ambaye ni hakimu katika mahakama ya Mwanzo Dodoma mjini Flora Mhelela ameieleza mahakama kuwa Pasificus alifika ofisini kwake wakati alipokuwa hakimu katika mahakama ya mwanzo ya Bomani iliyopo Iringa mjini kwa ajili ya maungamo juu ya kesi inayomkabili.

Ameiambia mahakama kuwa mnamo Septemba 05, 2012 mtuhumiwa kwa kuongozwa na askari ambaye hakumkumbuka jina, alifika ofisini kwake kwa ajili ya maungamo juu ya kesi inayomkabili ambapo ulikuwa ni muda wa saa 07:24 mchana.

Amesema baada ya kupata taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa utoaji maelezo mtuhumiwa alikiri kuwa amehiari mwenyewe kutoa maelezo ambapo baada ya kukaguliwa katika mwili wake alikutwa na kidonda kibichi kidoleni pamoja na majeraha makavu.

“Mtuhumiwa aliniambia kwamba mnamo Septemba 2, 2012 ilitokea kazi ambayo alipangiwa kwenda Nyololo ambako kulikuwa na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikwenda kufanya mkutano.

“Aliendelea kusema kuwa kama ilivyo kawaida kwa ajili ya ulinzi na usalama, kwamba hawakutakiwa kufanya mkutano huo kwa kuwa haukuwa rasmi. Mkutano ulikuwa unazuiliwa kwa sababu kulikuwa na tukio la sensa” ameeleza shahidi namba tatu.

Wednesday, February 4, 2015

VIJANA WAONYWA KUTOKUJIINGIZA KATIKA UFISADI



Jaji Mstaafu Raymond Mwaikasu

VIJANA Wakristo Wakatoliki wametakiwa kutokujiingiza katika vitendo vya ufisadi na badala yake wametakiwa kutumia uhuru waliopewa na Mungu ipasavyo bila kuwakwaza wengine na kwamba viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu katika haki ni wasaliti wasiowatakia mema wengine.

Haya yamezungumzwa na Jaji Mstaafu Raymond Mwaikasu alipokuwa akiwahutubia vijana wakati wa sherehe za mzimamizi wao Mt. Yohane Bosco zilizofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Parokia ya Mkwawa Jimbo lringa.

Jaji Mwaikasu amesema ufisadi umekuwa ni tatizo kubwa katika serikali ya Tanzania na kwamba unasababishwa na watu wasiyo na huruma, wabinafsi, wasiomuogopa Mungu kuwa waroho kupindukia.