TAASISI ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa iringa wamewataka wananchi kutokubali kuhongwa na wagombea wa uombozo katika kipindi hiki tunapoelekea katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Haya yamezungumzwa na ofisa wa TAKUKURU
elimu kwa umma Iringa Anneth Mwakatobe alipokuwa akiongea na mtandao huu
ofisini kwake.
Mwakatobe amewataka wananchi kutambua
viashiria vya rushwa wakati huu kuwa ni pamoja na mgombea au mwanasiasa kutoa
kitu kama khanga na vitenge kwa ajili ya kutaka kuchaguliwa ama kushawishi
wananchi kumchagua mtu fualani.
“Mgombea akiwa nakusanya baadhi ya watu
halafu anakutana nao kwa siri watu wengine kujua aidha kwa kutaka kuongea nao
labda kutoa ahadi kwa watu, ahadi ambazo zinawashawishi watu kumchagua au
kuwapa watu fedha ili wamchague ni rushwa.
“Pia mgombea ambaye hajiamini yaani
mgombea ambaye hana maslahi ya taifa, mgombea ambaye hana sera lakini haoneshi
kama ana nia ya dhati yaani anashawishi zaidi, huyo naye tunaweza kusema ana
viashiria vya rushwa” amesema Mwakatobe.
Amesema kipindi hiki ni kipindi cha
wananchi kuwa watulivu na kuwachunguza wanansiasa kwa umakini ili pale
utakapofika muda wa kuja kwao kuomba kuchaguliwa wawe na majibu sahihi.
Ameongeza kuwa viongozi wanaotumia njia
ya kuwarubuni wapiga kura kwa kuwahonga kitu chochote si wazalendo kwa kuwa
njia wanayoitumia si halali na kwamba wananchi wawakatae watu wa namna hiyo
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa TAKUKURU ili wakamatwe.
Hata hivyo amesema TAKUKURU hawatachoka
kutoa elimu kwa umma ili jamii iweze kutoa ushirikiano kupambana na vitendo vya
rushwa ambavyo vimekuwa vikiumiza wananchi.
“Moja ya kazi yetu ni kutoa elimu kwa
umma hasa wapiga kura katika kipindi kama hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi ili
tuweze kupata viongozi waaminifu, waadilifu na viongozi wazalendo.
“Tunawaomba wananchi kuwa makini kwani
elimu hii tunatumia njia mbalimbali kama vile semina, mikutano ya hadhara,
vipindi vya redio ikitokea na pia kufanya mijadala ya wazi kwa wananchi
mbalimbali na wadau ambapo kikubwa zaidi ni kutafut au kupata viongozi wa
waadilifu katika kipindi cha uchaguzi” amesema.
Amefafanua kuwa viongozi waadilifu ni
wale ambao wapo tayari kupambana na rushwa, ambao pia wako tayari kuleta
maendeleo kwenye jamii wanayoiongoza.
“Tunaaomba wananchi wasijihusishe kabisa
na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi na pia watanzania wawe wazalendo yaani
wawe wachungu na nchi yao.
“Watanzania wawe wajasiri, wasiwaogope
TAKUKURU, wasiwaogope viongozi wenye vitisho na wawe jasiri kutoa taarifa za
viongozi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na pia watanzania wajifunze
kuichukia rushwa” amesema.
No comments:
Post a Comment