KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Wednesday, May 20, 2015

Polisi wadaiwa kuua raia mmoja huku wawili wakijeruhiwa

NA MWANDISHI WETU, NJOMBE.

RAIA mmoja mkazi wa Njombe mjini ameuawa kwa risasi na Polisi kitendo kilichowatia hasira wananchi na kufunga mitaa kwa maandamano mkoani Njombe kwa kutaka kujua sababu zilizowafanya Polisi kufyatua risasi kwa wananchi na kusababisha kifo cha mwanachi huyo.

Kutokana na tukio hilo wananchi waliamua kufanya maandamano leo kutaka kujua sababu za mwezao kuuawa jambo lililosababisha jeshi la polisi kutumia mabomu na silaha za moto hapo na kujeruhi raia wengine wawili katika maandamano hayo.

Hasira za wananchi hao zimesababisha shughuli kusimama kwa siku nzima huku maduka yakifungwa pamoja na usafiri kuwa mgumu kutokana na wananchi kutaka kupata majibu ya kuuawa kwa  raia huyo.

Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wakazi wa Njombe wamesema Polisi walifika kilabuni walikokuwa wakinywa pombe wananchi na kufyatua risasi bila sababu yoyote kisha kumpiga mwananchi huyo aliyefariki dunia papo hapo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Amos Nziku ameeleza kuwa, ilikuwa majira ya jioni jana walipokuwa wakipata vinywaji katika kilabu kimoja cha pombe ambapo alitokea raia mmoja akaingia kilabuni hapo akikimbia jambo lililowashtusha na kumtaka kueleza sababu ya kuingia akiwa anakimbia.

“Jana tulikuwa kilabu cha Nyondo tukipata kiburudisho chetu cha koo huku tukiongea na marafiki gafla akaingia mtu akikimbia tukashtuaka sana. Sasa kule kushtuka kila mtu akataka kujua anakimbia nini, yule jamaa akatuambia polisi wanamfukuza.

“Tulitoka watu wote pale kilabuni kuangalia tukawaona kweli polisi tukaanza kuwapigia kelele kutaka kujua ni kwa nini wanamfukuza. Lengo ni kujua kama ni mwizi ili tumshughulikie lakini cha kushangaza, polisi wakaanza kufyatua risasi kuelekeza kwetu. Kwa bahati mbaya risasi ilimfikia mwenzetu mmoja akafariki papo hapo” amesema Nziku.

Monday, April 20, 2015

Zwelithini kutuliza raia Afrika Kusini

Goodwill Zwelithini, Mflame wa Zulu
Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo.

Mfalme huyo ameshutumiwa kwa kuchochea mashambulio hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu saba.

Zwelithini, alinukuliwa akisema kuwa raia wote wa kigeni wanapaswa kurejea katika mataifa yao.

Zaidi ya watu mia tatu wamekamatwa kuhusiana ghasia hizo.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kufurika uwanja mmoja ulioko mji wa Mashariki wa Durban kusikiliza hotuba hiyo ya Mfalme Zwelithini.

Amekariri kuwa matamshi yake hayakufahamika.

Miongoni mwa washukiwa waliokamatwa hivi karibuni na wanaume watatu ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.

Picha kadhaa zimeonyesha Emmanuel Sithole akindungwa kisu huku umati mkubwa ukitizama.

Raia moja wa kigeni akishambuliwa nchini Afrika Kusini
Mama mmoja raia wa kigeni ambaye nyumba yake ilivamiwa nchini Afrika Kusini

Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, amesema mashambulio hayo yanakwenda kinyume na maadili yote wanayoamini.

Makundi kadhaa yaliyojihami yameshambulia na kupora maduka kadhaa yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Huku idadi ya watu wasio na kazi nchini humo, ikikadiriwa kuwa zaidi ya asilimia Ishirini na nne, raia wengi wa taifa hilo wamewashutumu raia wa kigeni kwa kuchukua nafasi zao za kazi.

Maelfu ya raia hao wa kigeni, wamekimbia makwao na sasa wanaishi katika kambi za muda, ili hali mataifa jirani wameanza shughuli ya kuwahamisha raia wao.

Siku ya Jumapili, serikali ya Zimbabwe imetuma mabasi kadhaa mjini Durban kwenda kuwachukua raia wake wapatao mia nne.

Takwimu rasmi za serikali zinakadiria kuwa kuna raia milioni mbili wa kigeni wanaoishi nchini Afrika Kusini, lakini wengi wanahoji kuwa idadi hiyo huenda ni kubwa zaidi.

Chanzo: bbc swahili

Monday, April 13, 2015

Zitto: Viongozi wa vyama wasiwe viongozi wa serikali. > Wananchi wamwita msaliti

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kambwe akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema Chamani cha Mapinduzi kinashindwa kutofautisha uongozi wa chama na uongozi wa serikali na kusababisha kuwafanya wananchi kushindwa kujua utendaji wa viongozi hao.

Zitto ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa katika Mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.

Amesema si rahisi kujua utendaji wa kazi za chama na kazi sa serikali kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na kuwa na kofia mbili za uenyekiti wa chama taifa na kofia ya urai wan chi na kwamba haijulikani ni wakati gani anafanya kazi za chama na ni wakati gani anafanya kazi cha taifa.

Amesema nchi inakosa mwelekeo kutokana na kuwapo kwa mfumo wa uongozi wa kinyonyaji na dhuruma unaotokana na viongozi wasiokuwa na maadili ambao kazi yao ni kufanya unyonyaji badala ya kufanya kazi za taifa.

“Ifike mahali ikaeleweka na kutofautisha viongozi wa chama na viongozi wa serikali ili utendaji uweze kueleweka. Si rahisi kutambua Rais Kikwete ni wakati gani anafanya kazi za chama na ni wakati gani anafanya kazi za taifa.

“Mfumo wa uongozi wa namna hii ni wa kinyonyaji kwa kuwa viongozi wengi wanafanya kazi za kinyonyaji kwa kuwa hakuna wa kumkemea mwenzake. Ndiyo maana hata mafisadi wanatazamwa usoni tu kwa sababu mfumo wa uongozi ndivyo ulivyo” amesema.

Amesema mtu yeyote akisema yeye ni kiongozi lazima awe mpambanaji kupigania haki za watu wake kwa ajili ya kuhakikisha watu wake wanakuwa na maendeleo.

Amesema umasikini wa watanzania unasababishwa na wabunge wasiopamba kupigania haki za watu wao na kugeuka kuwa wanyonyaji wasio na huruma.

Amewataka watanzania kuwa kuelewa kuwa si kwamba ufisadi unakwisha bali unaendelea kwa kasi zaidi kwa kuwa serikali iliyopo madarakani imekosa meno kuwashughulikia wezi sugu wanaoiba mali ya umma na kwamba umasikini ni chaguo la viongozi wa kisiasa.

“Umasikini wa Tanzania ni chaguo la viongozi wa kisiasa. Tusipofanya mabadiliko sisi wananchi, umasikini huu utaendelea kuwapo na hautakoma kwa kuwa wenzetu wa chama tawala ndio chaguo lao” amesema.

Amesema tatizo kubwa uchumi umeshikiliwa na watu wachahe ambao hao hao ni viongozia wa kisiasa na wengine ni viongozi wa serikali na kwamba uchumi wa Iringa pia umeshikiliwa na watu wa namna hiyo.

Tuesday, March 24, 2015

Ndege ya Ujerumani yaanguka nchini Ufaransa

Ndege ya shirika la ndege la Germanwings
Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

 Chanzo: bbc swahili

Thursday, March 19, 2015

Wananchi wa Ndolezi waingiwa hofu ya kuvamiwa na simba



WANANCHI wa Mufindi katika Mkoa Iringa wapo katika taharuki kubwa na hofu ya kuvamiwa na simba kutokana na wanayama hao kupita katika maeneo mengi katika makazi yao.

Haya yamezungumzwa leo na mwenyekiti wa Kijiji cha Ndolezi Kata ya Boma katika wilaya ya Mundi, Clement Nditu alipokukuwa akiongea na mtandao huu juu ya taharuki inayokikumba kijiji chake.

Nditu amesema wanakijiji waligundua kuwa wapo hatarini walipokuwa wakienda mashambani mwao na kuona nyayo za mnayama wasiyemfahamu jambo lililowalazimu kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ili hatua za kiusalama zifuate.

Maelezo ya mwenyekiti wa kijiji hicho yanakuja baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kijiji cha Ndolezi kimevamiwa na simba japo kuwa haikuelezwa kama kuna madhara yoyote kwa wananchi.

Mtandao huu umemtafuta ofisa mtendaji wa kijiji hicho Yohana Kikungwe ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi ambapo amesema kijiji hicho na maeneo jirani katika Kata hiyo wapo katika sintofahamu ya hatima ya wanayama hao.

Tuesday, March 17, 2015

Hospitali ya Rufaa Iringa yakabiliwa na uhaba wa damu

UPATIKANAJI wa damu katika hospitali ya rufaa ya Iringa pamoja na hospitali za wilaya ni tete kutokana na benki ya damu kuishiwa damu.

Haya yamezungumzwa na mteknolojia wa maabara Mkoa wa Iringa Mlike Mwalongo alipotakuwa akihojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake leo juu ya upatikanaji wa damu.

Mwalongo amesema hali ya upatikanaji wa damu ni tete na kwamba hospitali ya rufaa Iringa pekee inahitaji wastaniwa  wa unit 210 kwa mwezi ambapo ni sawa na lita 105 kwa mwezi.

Amesema uhaba wa damu unatokana na kukosa vitenganishi (vitendea kazi) ambavyo vingewasaidia wataalam wa damu kufika maeno mbalimbali kwa ajili ya kuwaomba wananchi kuchangia.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni hali ya uchumi ambapo awali walikuwa wakitegemea wafadhili katika ukusanyaji wa damu kwa wanaochangia lakini kwa wakati huu wamekosa ufadhili na kusababisha damu kutopatikana kiurahisi.

“Hali ya upatikanaji wa damu kwa wakati huu ni tete. Damu haitolewi sehemu moja ila watu wanatembea sehemu mbalimbali kwa ajili ya kwenda kuomba na kutoa damu kwa watu mbalimbali wanaoguswa na kuchangia.

“Pia tuna uhaba wa dawa za kupimia damu. Kwa kuwa upatikanaji wa damu ni tete, tunatumia mbadala kupata damu ili kumuokoa mgonjwa kwa kuwaomba ndugu wa mgonjwa achangie mgonjwa wake vinginevyo hatuna jinsi” amesema Mwalongo.

Anabainisha kuwa tatizo la damu linaloikumba hospitali ya rufaa Iringa ni tatizo la kanda nzima ya nyanda za juu kusini inayojumuisha mikoa sita ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

Kwa mujibu wa Mwalongo hospitali ya rufaa Iringa hutumia unit 6 hadi 7 kwa siku ambapo ni sawa na kutumia lita 3.5 kwa siku.

Saturday, March 14, 2015

TAKUKURU wataka wananchi wasikubali kuhongwa


TAASISI ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa iringa wamewataka wananchi kutokubali kuhongwa na wagombea wa uombozo katika kipindi hiki tunapoelekea katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Haya yamezungumzwa na ofisa wa TAKUKURU elimu kwa umma Iringa Anneth Mwakatobe alipokuwa akiongea na mtandao huu ofisini kwake.

Mwakatobe amewataka wananchi kutambua viashiria vya rushwa wakati huu kuwa ni pamoja na mgombea au mwanasiasa kutoa kitu kama khanga na vitenge kwa ajili ya kutaka kuchaguliwa ama kushawishi wananchi kumchagua mtu fualani.

“Mgombea akiwa nakusanya baadhi ya watu halafu anakutana nao kwa siri watu wengine kujua aidha kwa kutaka kuongea nao labda kutoa ahadi kwa watu, ahadi ambazo zinawashawishi watu kumchagua au kuwapa watu fedha ili wamchague ni rushwa.

“Pia mgombea ambaye hajiamini yaani mgombea ambaye hana maslahi ya taifa, mgombea ambaye hana sera lakini haoneshi kama ana nia ya dhati yaani anashawishi zaidi, huyo naye tunaweza kusema ana viashiria vya rushwa” amesema Mwakatobe.