WANACHI jijini Dar
es Salaam wanahofia usalama wao kutokana na kikundi cha uvamizi na upora “Panya
Road” ambacho kilizua taharuki jana katika maeneo mbalimbali jijini humu.
Ikiwa ni siku moja
tu baada ya kikundi hicho kudaiwa kujitokeza na kuvamia baadhi ya maeneo,
wananchi wanafanya shughuli zao kwa hofu juu ya usalama wao.
Mtandao huu
umepita maeneo ya Kimara na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hofu kuvamiwa
wapo katika shghuli zao za kila siku.
Majira ya saa moja
usiku jana katika maeneo ya Kimara wananchi walilazimika kusitisha shughli zao
mapema na kukimbilia majumbani mwao baada ya kuzagaa kwa taarifa mitaani kuhusu
kuzuka kwa kikundi hicho.
Usafiri ulikuwa
mgumu huku baada ya watoa huduma hiyo kulazimika kusitisha huduma kwa hofu ya
kikundi hicho huku watu wakikimbizana kila kona.
Taarifa hizo
zilisambaa kwa njia ya mitandao ya simu watu kutumiana ujumbe mfupi (sms), mitandao
mbalimbali ya kijamii pamoja na baadhi ya watu kupita wakiwatangazia watu kuwa
na tahadhari ju ya kikundi hicho.
Kikundi hicho
kinadaiwa kuvamia maeneo
mbalimbali na kupora vitu, ikiwemo maeneo ya Sinza na Mwananyamala, pamoja na
kujeruhi watu.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova akizungumzia taarifa kikundi hicho kupitia
kituo cha TBC1 hapo jana alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuwa na amani kwa kuwa kikundi hicho kina wahalifu wachache
na jeshi la polisi limekamata wawili ambao wamekamatwa na msako unaendelea.
“Sisi
kama Jeshi la Polisi tumepata taarifa vilevile kama walivyopata watu wengine, kwamba
hao vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ walikuwa wamezagaa maeneo mengi.
“Hawa
ni vijana ambao hawana kazi, hawana maadili mazuri kwanza tuzungumzie uzito wa
tatizo, jinsi ambavyo habari zilivyovuma zimevumishwa kubwa zaidi kuliko uzito
wa tukio lenyewe. Nataka niwaambie wananchi kwamba endeleeni na shughuli zenu” alisema
Kova.
Alikiri kuwapo kwa
kikndi hicho na kuwataka wananchi kuwa na amani kwa kutokana na jeshi la polisi
kuendesha msako kila kona katika jiji la Dar es Salaam.
“Hatukatai kwamba hawa vijana wapo.. lakini nasema suala limekuzwa
limetiwa hofu, watu wamepata hofu kupindukia.
Tutashughulikia suala la ‘Panya road’ na leo doria inaendelea usiku
kucha, wananchi waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo. Haiwezekani panya road
wakatawala Dar es Salaam… Haiwezekani panya road wawe na nguvu kuliko jeshi la
Polisi. Wamekamatwa wawili…
tuliwakamata muda mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao na tunaendelea kwasaka
wengine” alisema Kova.
No comments:
Post a Comment