KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Sunday, December 14, 2014

Uchaguzi Serikali za Mitaa waingia dosari Ngome



UCHAGUZI wa serikali za Mitaa katika Mtaa wa Ngome Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa umeanza kwa dosari licha ya kulazimika kuanza saa 6:04 mchana kutokana na kucheleweshwa vifaa vya kupigia kura.

Licha ya vifaa vya kupigia kura kuchelewa, bado ilitokea dosari katika karatasi za kupigia kura kwa kile kilochoonekana kwa baadhi ya majina ya waliogombea ujumbe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoonekana kwenye karatasi za kupigia kura na badala yake yakaingizwa majina ya watu wengine ambao hawakujaza fomu za kugombea.

Sambamba na hilo kwa upande wa wagombea kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa na kosa la waliogomea viti maalum kuingizwa jina la mwanaume aliyegombea ujumbe huku mwanamke aliyegombea viti maalumu uingizwa kwenye karatasi la wagombea wa ujumbe.

Sababu hizi zimemlazimu wakala wa Chadema kutokubaliana na utaratibu huo na kutaka utolewe ufafanuzi zaidi kabla ya kuanza zoezi la upigaji kura na kumlazimu msimamizi wa uchaguzi wa kituo hicho kumpigia simu ofisa mtendaji wa Kata ili aweze kutolea ufafanuazi  jambo ambalo pia lilimlazimu ofisa mtendaji kurudisha karatasi kwa mkurugenzi ili zifanyiwe marekebisho.

Baada ya maelezo ya ofisa mtendaji wa Kata ya Kihesa Wilbert Chahe kuwa kuna makosa katika karatasi hizo, wananchi walipandisha hasira na kumzingira ofisa huyo jambo lililowawalazimu vijana wa Chadema kumnusuru ili aweze kurudisha karatasi zikarekebishwe.

Tuesday, December 9, 2014

Watanzania waadhimisha miaka 53 ya Uhuru

Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere
Tanzania bara leo inaadhimisha miaka 53 toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.
Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Ni miaka 53 tangu Tanzania ijipatie uhuru wake, lakini hali za Watanzania wengi bado ni duni, kiuchumi na kijamii.

Chanzo: bbc swahili

Wednesday, October 15, 2014

WANANCHI WAMTAKA DIWANI AJIUZULU UDIWANI KABLA HAJANG'OLEWA KINGUVU



Jengo la shule ya sekondari ya Kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa linavyozidi kuharibika huku likijengwa ambalo wananchi wanamtaka diwani na afisa mtendaji wao wa Kata kuachia ngazi. Hapa ni kwa upande wa nadani.


Hapa ni sehemu ya upande wa ndani wa jengo lililopasuka nyufa.


Hapo ni upande wa nje wa njengo hilo ambalo limesusiwa na wananchi baada ya kuonekana linafanyiwa hujuma katika ujenzi na kujengwa chini ya kiwango.



WANANCHI wa Kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa wamepanga kumshtaki Diwani wao Mejus Mgeveke (CCM) pamoja na kumtaka ajihuzulu nafassi hiyo mara moja kabla hawajamng’oa kwa kile wanachomtuhumu kuhujumu ujenzi wa shule ya Kata.

Wananchi wamefikia uamuzi huo kutokana na jengo la shule ya Kata hiyo kuwa mashakani kuanguka baada ya kupasuka na nyufa siku baada ya siku huku likiendelea kujengwa.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Kijiji cha Kimala Diwani hakutakiwa kuzungumza chochote kuhusiana na ujenzi huo baada ya wananchi kumtaka kukaa kimya kwa kile walichoeleza kuwa alishindwa kutoa taarifa sahihi tangu awali na kwamba hali ya jengo ni mbaya.

Katika hali isiyo ya kawaida wakati wa Mkutano huo wananchi walikuwa tayari kumchapa Diwani huyo pamoja na afisa mtendaji wa Kata kwa tuhuma ya kushirikiana kuhujumu ujenzi wa shule hiyo ambayo ilikuwa ni tegemeo la ukombozi wa elimu katika Kata hiyo.

“Hatuhitaji taarifa yoyote kuhusiana na jengo lililojengwa kihuni, jengo hilo wabaki nalo diwani na afisa mtendaji wa Kata kwa sababu wamelijenga wao. Tumetumia nguvu kubwa lakini wenzetu wakatuona wapumbavu. Tupo tayari kuanza jengo linguine lakini siyo hilo” walisema wananchi katika mkutano huo.

Pia wamesema hawapo tayari kuona diwani huyo akifanya kazi katika Kata hiyo kwa kuwa hawamtaki tena kumuona kwa kuwa amewadharau kwa kiasi kikubwa.

Katika mkutano uliofanyika tena juzi katika kijiji cha Kimala mwenyekiti wa kijiji hicho Sadrus Lwanzali aliweza kukubaliana na wananchi kuwa diwani huyo anapaswa kuachia madaraka kabla kipute cha kumng’oa hakijaanza.

“Kama atakaidi agizo letu tutamtoa kama tulivyomuamini kwa mara ya kwanza. Tutafanya kila litakalowezekana kuhakikisha anang’ooka kama yeye mwenyewe hataki kujingoa. Tunachotaka aondoke kwa hiari tu ila kama hataki tutamng’oa, maana atakuwa ametudharau kwa mara nyingine” walisema wananchi.

Kila wakati katika mkutano huo zilikuwa zikisikika ksauti za watu wakisema “anasubiri nini kujitokeza hapa ajiweke pembeni mwenyewe?” hali ambayo ilionesha wananchi kuwa na hasira muda wote.

Alipotakiwa kutoa maelezo juu ya tyhuma zinazomkabili diwani huyo alisema hajafanya kazi kwa ubinafsi bali kazi ilifanyika kwa kufuata taratibu zote.

"Siyo kama wanavyonithumu bali kazi ya ujenzi wa shule hii umefuata taratibu zote kuanzia wilayani hadi mkoani kwa kuzingatia maagizo yote. hiyo ni bahati mbaya tu inatokea" alisema Mgeveke.

Hii ni mara ya tatu kwa wananchi wa kata hiyo kuibuka na suala la jengo hilo ambapo mara ya kwanza nay a pili diwani huyo aliweza kuziba nyufa zilizopasuka katika jengo hilo lakini zikiendelea kupasuka tena huku mara hii zikiongezeka zaidi na jengo kuanza kutitia na kupinda kuta kama dalili ya kuanza kuanguka.

Sunday, September 21, 2014

WAHUDUMU WA AFYA WAFANYA KAZI GIZANI KIJIJINI

Zahanati ya kijiji cha Rungemba

WAHUDUMU wa afya katika zahanati ya Rungemba Kata ya Rungemba Wilaya ya Mufindi katika Mkoa wa Iringa wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi nyakati za usiku kwa sababu ya kukosa mwanga.

Hayo yamebainishwa na muuguzi katika zahanati hiyo Suzan Mhongole alipokuwa akiongea na gazeti hili jana juu ya ugumu wa kazi yao nyakati za usiku.

Mhongole amesema wanalazimika kutumia kurunzi nyakati za usiku hasa pale anapofika mama mjamzito mwenye uchungu wa kujifungua au mgonjwa anayehitaji huduma ya haraka.

“Tulikuwa na mwanga unaotokana na jua (solar power) lakini zimeharibika na hatujui tatizo ni nini kwani hata wakija mafundi hawatuelezi tatizo ili ufanyike utaratibu wa kutatua tatizo hilo.