Hapa ni sehemu ya upande wa ndani wa jengo lililopasuka nyufa.
Hapo ni upande wa nje wa njengo hilo ambalo limesusiwa na wananchi baada ya kuonekana linafanyiwa hujuma katika ujenzi na kujengwa chini ya kiwango.
WANANCHI wa Kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa wamepanga kumshtaki Diwani wao Mejus Mgeveke (CCM) pamoja na kumtaka ajihuzulu nafassi hiyo mara moja kabla hawajamng’oa kwa kile wanachomtuhumu kuhujumu ujenzi wa shule ya Kata.
Wananchi wamefikia uamuzi huo kutokana na jengo la shule ya Kata hiyo kuwa mashakani kuanguka baada ya kupasuka na nyufa siku baada ya siku huku likiendelea kujengwa.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Kijiji cha Kimala Diwani hakutakiwa kuzungumza chochote kuhusiana na ujenzi huo baada ya wananchi kumtaka kukaa kimya kwa kile walichoeleza kuwa alishindwa kutoa taarifa sahihi tangu awali na kwamba hali ya jengo ni mbaya.
Katika hali isiyo ya kawaida wakati wa Mkutano huo wananchi walikuwa tayari kumchapa Diwani huyo pamoja na afisa mtendaji wa Kata kwa tuhuma ya kushirikiana kuhujumu ujenzi wa shule hiyo ambayo ilikuwa ni tegemeo la ukombozi wa elimu katika Kata hiyo.
“Hatuhitaji taarifa yoyote kuhusiana na jengo lililojengwa kihuni, jengo hilo wabaki nalo diwani na afisa mtendaji wa Kata kwa sababu wamelijenga wao. Tumetumia nguvu kubwa lakini wenzetu wakatuona wapumbavu. Tupo tayari kuanza jengo linguine lakini siyo hilo” walisema wananchi katika mkutano huo.
Pia wamesema hawapo tayari kuona diwani huyo akifanya kazi katika Kata hiyo kwa kuwa hawamtaki tena kumuona kwa kuwa amewadharau kwa kiasi kikubwa.
Katika mkutano uliofanyika tena juzi katika kijiji cha Kimala mwenyekiti wa kijiji hicho Sadrus Lwanzali aliweza kukubaliana na wananchi kuwa diwani huyo anapaswa kuachia madaraka kabla kipute cha kumng’oa hakijaanza.
“Kama atakaidi agizo letu tutamtoa kama tulivyomuamini kwa mara ya kwanza. Tutafanya kila litakalowezekana kuhakikisha anang’ooka kama yeye mwenyewe hataki kujingoa. Tunachotaka aondoke kwa hiari tu ila kama hataki tutamng’oa, maana atakuwa ametudharau kwa mara nyingine” walisema wananchi.
Kila wakati katika mkutano huo zilikuwa zikisikika ksauti za watu wakisema “anasubiri nini kujitokeza hapa ajiweke pembeni mwenyewe?” hali ambayo ilionesha wananchi kuwa na hasira muda wote.
"Siyo
kama wanavyonithumu bali kazi ya ujenzi wa shule hii umefuata taratibu
zote kuanzia wilayani hadi mkoani kwa kuzingatia maagizo yote. hiyo ni
bahati mbaya tu inatokea" alisema Mgeveke.
Alipotakiwa
kutoa maelezo juu ya tyhuma zinazomkabili diwani huyo alisema hajafanya
kazi kwa ubinafsi bali kazi ilifanyika kwa kufuata taratibu zote.
Hii ni mara ya tatu kwa wananchi wa kata hiyo kuibuka na suala la jengo hilo ambapo mara ya kwanza nay a pili diwani huyo aliweza kuziba nyufa zilizopasuka katika jengo hilo lakini zikiendelea kupasuka tena huku mara hii zikiongezeka zaidi na jengo kuanza kutitia na kupinda kuta kama dalili ya kuanza kuanguka.
No comments:
Post a Comment