WAKATI Serikali ya awamu ya tano ikija
na neon utumbuaji majipu, baadhi ya watendaji wamekwepa kuita rushwa au takrima
na kubuni jina linguine kuwa ni “mipango”.
Mtandao huu umeshuhudia baadhi ya
maofisa watendaji wakitaka kupa fedha kutoka kwa mwanamke mmoja aliyekuwa
akijenga kiti cha nyumba katika mtaa wa Igumbilo Kata ya Ruaha katika Manispaa
ya Iringa wakidai kuwa za mipango.
Wakati watendaji hao wakimkomalia
mwanamke huyo ili awapatie fedha, walikuwa wakitumia kigezo kuwatamsimamisha
asiendelee na ujenzi kwa sababu ya kutokuwa na kibali.
Wakati wakiendelea kumkomalia mama huyo mtandao huu ulitaka kujua kama hizo fedha ambazo angezitoa mama huyo
zinatolewa stakabadhi na kama ni za kisheria lakini ofisa mtendaji wa mtaa huo
Ashery Msigala alisisitiza kuwa ni kwa ajili ya mipango.
“Siku zote ukitaka kufanikiwa kwa haraka
lazima uwe na mipango. Ukitaka kufanyiwa kazi yako kwa haraka zaidi lazima uwe
na mipango.
“Unapoamka kwenda ofisi ya mtu kwa ajili
ya kupata huduma, ili huduma hiyo iweze kwenda kwa haraka zaidi lazima
unapoondoka uwe na mipango kama hamasa kwa mtendaji unayekwenda kuonana naye
ili akusaidie” amesema Msigala.