Mwanamke mmoja amefariki na zaidi ya wanafunzi 20 kujeruhiwa katika oparesheni ya kuiga shambulio la kigaidi ilioendeshwa nchni kenya, katika chuo kikuu cha Strathmore.
Oparesheni
hii ilipangwa na chuo hicho pamoja maafisa wa polisi bila kuarifu
wanafunzi na wafanyakazi, ili kubaini ikiwa chuo hicho kiko tayari
kukabiliana na tukio la kigaidi.
Kauli rasmi kutoka chuo kikuu cha
strathmore, imedhibitisha kwamba mfanyakazi mmoja amefariki kutokana na
majeraha aliyopata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya tatu.
Wanafunzi zaidi ya ishirini wamejeruhiwa wanne kati yao wakiwa hali mahututi baada ya mkanyagano
mkanyangano huo ulisababishwa na mkakati wa usalama uliokuwa ukiendeshwa chuoni humo na vikosi vya usalama.
Wengi waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitalini jijini Nairobi akiwemo mhadhiri aliyeruka kutoka ghorofa ya nne waliumia miguu na mikono katika harakati za kuruka kupitia madirisha na milango wakati wa tukio hilo.
Mkakati huo ulipaswa kuangazia maandalizi ya wanafunzi na watu wengine endapo tukio la kigaidia linaweza tokea.
Hata
hivyo usimamizi wa chuo hicho umeelezea kusikitishwa na jinsi tukio
hilo lilivyozuka na kusababisha majeraha huku ukiahidi kuwalipia gharama
za hospitali za wote waliojeruhiwa.
Tukio hili linajiri miezi
kadhaa baada ya wapiganaji wa al shabaab kutekeleza shambulio la kigaidi
mwezi aprili katika chuo kikuu cha Garrissa, na kusababisha vifo vya
wanafunzi mia moja arobaini na saba
Chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment