KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Monday, November 30, 2015

Shambulio bandia laleta maafa Kenya

Mwanamke mmoja amefariki na zaidi ya wanafunzi 20 kujeruhiwa katika oparesheni ya kuiga shambulio la kigaidi ilioendeshwa nchni kenya, katika chuo kikuu cha Strathmore.

Oparesheni hii ilipangwa na chuo hicho pamoja maafisa wa polisi bila kuarifu wanafunzi na wafanyakazi, ili kubaini ikiwa chuo hicho kiko tayari kukabiliana na tukio la kigaidi.

Kauli rasmi kutoka chuo kikuu cha strathmore, imedhibitisha kwamba mfanyakazi mmoja amefariki kutokana na majeraha aliyopata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya tatu.

Wanafunzi zaidi ya ishirini wamejeruhiwa wanne kati yao wakiwa hali mahututi baada ya mkanyagano
mkanyangano huo ulisababishwa na mkakati wa usalama uliokuwa ukiendeshwa chuoni humo na vikosi vya usalama.

Wengi waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitalini jijini Nairobi akiwemo mhadhiri aliyeruka kutoka ghorofa ya nne waliumia miguu na mikono katika harakati za kuruka kupitia madirisha na milango wakati wa tukio hilo.

Mkakati huo ulipaswa kuangazia maandalizi ya wanafunzi na watu wengine endapo tukio la kigaidia linaweza tokea.

Hata hivyo usimamizi wa chuo hicho umeelezea kusikitishwa na jinsi tukio hilo lilivyozuka na kusababisha majeraha huku ukiahidi kuwalipia gharama za hospitali za wote waliojeruhiwa.

Tukio hili linajiri miezi kadhaa baada ya wapiganaji wa al shabaab kutekeleza shambulio la kigaidi mwezi aprili katika chuo kikuu cha Garrissa, na kusababisha vifo vya wanafunzi mia moja arobaini na saba


Chanzo: bbc swahili

Papa 'wakristu wasilipize kisasi' Afrika ya Kati

Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.

Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu.

Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa Anti-Balaka.

Asili mia kubwa ya takriban waislamu laki moja nchini humo, walikimbia mji huo kufuatia mapigano yaliyodumu kwa ziaidi ya miaka mitati.

Misikiti mingi iliharibiwa wakati wa vita hivyo.

Papa Francis amewataka wasameheane na waache kulipiza kisasi.

''Wakristo na Waislamu ni ndugu ,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.

''hatupaswi kulipiza kisasi na kumdhuru mtu yeyote kwa jina la mungu'' alisema Papa Francis.

Hivi sasa leo Papa Francis anaongoza misa yake ya mwisho barani Afrika katika uwanja mkuu wa kitaifa ambako anatarajiwa kutoa wito wa maridhiano, amani na utengamano.