KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Monday, April 20, 2015

Zwelithini kutuliza raia Afrika Kusini

Goodwill Zwelithini, Mflame wa Zulu
Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo.

Mfalme huyo ameshutumiwa kwa kuchochea mashambulio hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu saba.

Zwelithini, alinukuliwa akisema kuwa raia wote wa kigeni wanapaswa kurejea katika mataifa yao.

Zaidi ya watu mia tatu wamekamatwa kuhusiana ghasia hizo.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kufurika uwanja mmoja ulioko mji wa Mashariki wa Durban kusikiliza hotuba hiyo ya Mfalme Zwelithini.

Amekariri kuwa matamshi yake hayakufahamika.

Miongoni mwa washukiwa waliokamatwa hivi karibuni na wanaume watatu ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.

Picha kadhaa zimeonyesha Emmanuel Sithole akindungwa kisu huku umati mkubwa ukitizama.

Raia moja wa kigeni akishambuliwa nchini Afrika Kusini
Mama mmoja raia wa kigeni ambaye nyumba yake ilivamiwa nchini Afrika Kusini

Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, amesema mashambulio hayo yanakwenda kinyume na maadili yote wanayoamini.

Makundi kadhaa yaliyojihami yameshambulia na kupora maduka kadhaa yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Huku idadi ya watu wasio na kazi nchini humo, ikikadiriwa kuwa zaidi ya asilimia Ishirini na nne, raia wengi wa taifa hilo wamewashutumu raia wa kigeni kwa kuchukua nafasi zao za kazi.

Maelfu ya raia hao wa kigeni, wamekimbia makwao na sasa wanaishi katika kambi za muda, ili hali mataifa jirani wameanza shughuli ya kuwahamisha raia wao.

Siku ya Jumapili, serikali ya Zimbabwe imetuma mabasi kadhaa mjini Durban kwenda kuwachukua raia wake wapatao mia nne.

Takwimu rasmi za serikali zinakadiria kuwa kuna raia milioni mbili wa kigeni wanaoishi nchini Afrika Kusini, lakini wengi wanahoji kuwa idadi hiyo huenda ni kubwa zaidi.

Chanzo: bbc swahili

Monday, April 13, 2015

Zitto: Viongozi wa vyama wasiwe viongozi wa serikali. > Wananchi wamwita msaliti

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kambwe akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema Chamani cha Mapinduzi kinashindwa kutofautisha uongozi wa chama na uongozi wa serikali na kusababisha kuwafanya wananchi kushindwa kujua utendaji wa viongozi hao.

Zitto ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa katika Mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.

Amesema si rahisi kujua utendaji wa kazi za chama na kazi sa serikali kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na kuwa na kofia mbili za uenyekiti wa chama taifa na kofia ya urai wan chi na kwamba haijulikani ni wakati gani anafanya kazi za chama na ni wakati gani anafanya kazi cha taifa.

Amesema nchi inakosa mwelekeo kutokana na kuwapo kwa mfumo wa uongozi wa kinyonyaji na dhuruma unaotokana na viongozi wasiokuwa na maadili ambao kazi yao ni kufanya unyonyaji badala ya kufanya kazi za taifa.

“Ifike mahali ikaeleweka na kutofautisha viongozi wa chama na viongozi wa serikali ili utendaji uweze kueleweka. Si rahisi kutambua Rais Kikwete ni wakati gani anafanya kazi za chama na ni wakati gani anafanya kazi za taifa.

“Mfumo wa uongozi wa namna hii ni wa kinyonyaji kwa kuwa viongozi wengi wanafanya kazi za kinyonyaji kwa kuwa hakuna wa kumkemea mwenzake. Ndiyo maana hata mafisadi wanatazamwa usoni tu kwa sababu mfumo wa uongozi ndivyo ulivyo” amesema.

Amesema mtu yeyote akisema yeye ni kiongozi lazima awe mpambanaji kupigania haki za watu wake kwa ajili ya kuhakikisha watu wake wanakuwa na maendeleo.

Amesema umasikini wa watanzania unasababishwa na wabunge wasiopamba kupigania haki za watu wao na kugeuka kuwa wanyonyaji wasio na huruma.

Amewataka watanzania kuwa kuelewa kuwa si kwamba ufisadi unakwisha bali unaendelea kwa kasi zaidi kwa kuwa serikali iliyopo madarakani imekosa meno kuwashughulikia wezi sugu wanaoiba mali ya umma na kwamba umasikini ni chaguo la viongozi wa kisiasa.

“Umasikini wa Tanzania ni chaguo la viongozi wa kisiasa. Tusipofanya mabadiliko sisi wananchi, umasikini huu utaendelea kuwapo na hautakoma kwa kuwa wenzetu wa chama tawala ndio chaguo lao” amesema.

Amesema tatizo kubwa uchumi umeshikiliwa na watu wachahe ambao hao hao ni viongozia wa kisiasa na wengine ni viongozi wa serikali na kwamba uchumi wa Iringa pia umeshikiliwa na watu wa namna hiyo.