KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Saturday, January 3, 2015

Dar wafanya kazi kwa hofu >Wahofia "panya road" >Wafanya kazi wakihofia kuvamiwa


WANACHI jijini Dar es Salaam wanahofia usalama wao kutokana na kikundi cha uvamizi na upora “Panya Road” ambacho kilizua taharuki jana katika maeneo mbalimbali jijini humu.

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kikundi hicho kudaiwa kujitokeza na kuvamia baadhi ya maeneo, wananchi wanafanya shughuli zao kwa hofu juu ya usalama wao.

Mtandao huu umepita maeneo ya Kimara na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hofu kuvamiwa wapo katika shghuli zao za kila siku.

Majira ya saa moja usiku jana katika maeneo ya Kimara wananchi walilazimika kusitisha shughli zao mapema na kukimbilia majumbani mwao baada ya kuzagaa kwa taarifa mitaani kuhusu kuzuka kwa kikundi hicho.

Usafiri ulikuwa mgumu huku baada ya watoa huduma hiyo kulazimika kusitisha huduma kwa hofu ya kikundi hicho huku watu wakikimbizana kila kona.