BARAZA la wanawake wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Bawacha) Mkoa wa Iringa wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yati cha Mersino Meraddin Migoli pamoja na fedha tasilimu kiasi cha shilingi 1,645,000/=.
Msaada huo umetolewa wakati walipotembelea kituoni hapo kama ni sehemu ya kufanya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika.
Wakikabidhi msaada huo, Mbunge wa viti maalum wa jimbo la Mjini Magharibi – Zanzibar Maryam Salum Msabaha alibubujikwa na machozi baada ya kuwaona watoto hao na kutoa msaada wa shilingi milioni moja huku Mbunge wa viti maalum Naomi Kaihula akitoa kiasi cha shlingi 550,000/=.
Akizungumza kituoni hapo Maryam Msabaha alisema jamii ina jukumu la kuishi na watoto wasio na wazazi kama familia ili kuwajenge uwezo wa kutengeneza maisha yao kimalezi.
Alisema suala la kulea watoto si la wamisionari pekee bali ni jukumu la kila mtu aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu na kwamba watoto wasibaguliwe.