KLERUU

KLERUU
KLERUU

Ibada

Ibada

Thursday, May 26, 2016

Maandamano ya kumpinga Kabila yafanyika DRC

Waandamana Kumpiga kabila
Maandamano ya upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa Upinzani Moise Katumbi.

Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.

Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.

Friday, May 20, 2016

Chanjo imepunguza viwango vya watoto wanaofariki
Umri wa kuishi barani Afrika unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani kulingana na shirika la afya dunia WHO.

Ripoti ya WHO inasema tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10 zaidi.Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.

Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.

Daktari Ties Boerma kutoka WHO ameimbia Newsday kwamba sababu moja ni kupungua kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.

Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:

Walioua watu msikitini Mwanza wasakwa

Shambulio lilitekelezwa wakati wa swala jioni
Polisi nchini Tanzania wanawazuilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika shambulio katika msikiti mmoja mjini Mwanza magharibi mwa nchi hiyo.

Watu watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi jijini humo, Ahmed Msangi, uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia mapanga na kuongeza kuwa, polisi wanachunguza chanzo cha shambulizi hilo.

Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, wamesema shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wasiopungua 15.
Hakuna aliyedai kuhusika katika shambulio hilo.

Tukio jingine la mauaji ya kutumia silaha pia limetokea katika mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga ambapo askari polisi aliyefahamika kwa jina la Sajenti Kinyogoli ameuawa na watu wasiojulikana.

Matukio hayo yote yametokea wiki hii kulipoibuka taarifa kwenye mtandao wa Twitter juu ya kikundi kilichojitambulisha kama wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa Islamic State wakifanya mazoezi eneo la Tanga, kaskazini mashariki mwa Tanzania.


Chanzo: bbc swahili

Monday, May 16, 2016

Kagame: Hatuwezi kumkamata Bashir

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza kwamba hakuna sababu hata moja itakayoifanya nchi yake kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir ikiwa ataalikwa kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kitakachofanyika nchini Rwanda mwezi Julai mwaka huu.

Rais Bashir anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na mauaji katika jimbo la Darfur.

Rwanda si mwanachama wa mahakama ya ICC.

Kutoka Kigali Yves Bucyana anaarifu.

Tuesday, May 10, 2016

Huduma ya mabasi ya mwendo wa kasi yaanza Dar


Abiria wakiwa wamepanda basi la BRT
Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.

Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.

ASiku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.

Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.

Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.

Chanzo: bbc swahili